Posts

Showing posts from April, 2025

TANZANIA KUNA WANAWAKE WAZURI SIJUI KWANINI JUX KAENDA KUOA NIGERIA

Image
    Katika kile kinachoonekana kuwa hisia za mshangao na mapenzi ya dhati kwa uzuri wa wanawake wa Tanzania, msanii maarufu Harmonize ametoa kauli kali kwenye ukurasa wake wa Instagram. Akiwa amevutiwa na video za harusi ya Juma, Harmonize ameandika: “MAN I JUST SAW THE VIDEOS OF THE WEDDING, TANZANIAN WOMEN ARE BEAUTIFUL, BOMBCLAAAAAAAT! One can ask themselves, why did Juma go all the way to Nigeria while the light is shining right here at home!” Kauli hiyo imezua mjadala mtandaoni, huku wengi wakikubaliana naye na wengine wakimtetea Juma kwa chaguo lake la mapenzi. Kama ilivyo kawaida ya Harmonize, alimalizia ujumbe wake kwa maneno yenye uzito: “Love is a beautiful thing” Je, una mtazamo gani kuhusu hili? Je, kweli mwanga ulikuwa hapa nyumbani? Toa maoni yako hapa chini na endelea kutembelea Dengah Media TZ kwa habari motomoto kama hizi!

PAPAYA EX AZUA TAHARUKI KWENYE HARUSI YA PRISCILLA OJO – AVAA VAZI LENYE PICHA YA BWANA HARUSI KIFUANI

Image
  Katika harusi ya kifahari iliyofanyika Lagos, Nigeria tarehe 17 Machi 2025, Priscilla Ojo – mwana wa muigizaji mashuhuri Iyabo Ojo – alifunga ndoa ya kitamaduni na mpenzi wake kutoka Tanzania, Juma Jux. Tukio hilo lilihudhuriwa na mastaa wengi wa Afrika, lakini lililowashangaza wengi zaidi ni tukio la Papaya Ex, mrembo maarufu na mjasiriamali wa mitandaoni. Papaya Ex alitinga harusini akiwa amevaa vazi lenye picha ya Juma Jux (bwana harusi) kifuani, na picha ya Priscilla (bibi harusi) kiunoni. Wakati wa sherehe, alitoka na kuanza kumwagia maharusi pesa huku vazi lake likiwa wazi kabisa kwa kila mtu kuona. Hali hiyo ilimkasirisha Priscilla ambaye alimkabili kwa swali, “Kwa nini umeweka picha ya mume wangu kifuani?” Papaya Ex alimjibu kwa utulivu, “Samahani baby, ni kwa sababu nakupenda.” Baadaye alieleza kuwa alifanya hivyo kwa ajili ya kupata attention mitandaoni. Harusi hiyo ilihudhuriwa na mastaa kama Diamond Platnumz, Mercy Aigbe, Peter Okoye, Ebenezer Obey, Femi Adebayo, na w...

JINSI NILIVYOKUTANA NA MUME WANGU JUMA JUX’ – PRISCILLA OJO

Image
 Priscilla Ojo, binti wa mwigizaji maarufu wa Nigeria Iyabo Ojo, amefunguka kuhusu jinsi alivyokutana na mume wake, msanii maarufu wa Tanzania, Juma Jux. Katika video ya mahojiano inayotrend mitandaoni, alieleza kuwa walikutana kwa mara ya kwanza kwenye safari ya kibiashara nchini Rwanda. Alisema: Tulikutana kwenye safari ya kibiashara nchini Rwanda, aliniona kwanza kwenye daraja la biashara (business class), halafu tukakutana tena hotelini. Alinipa namba yake na kuniambia nimtume ujumbe lakini sikufanya hivyo. Lakini baadaye alijua namna ya kunifikia na tukaanza kuzungumza.” Uhusiano wao uliendelea na hatimaye kupelekea harusi ya kitamaduni iliyofanyika Lagos, Nigeria, tarehe 17 Aprili 2025, baada ya kufunga ndoa ya Kiislamu nchini Tanzania mwezi Februari.JP2025: ‘Jinsi nilivyokutana na mume wangu Juma Jux’ – Priscilla Ojo Harusi hiyo imekuwa gumzo kubwa mitandaoni, na baadhi ya watu wakiiita "harusi ya mwaka," huku ikilinganishwa na harusi ya msanii Davido.

HARUSI ZA KISASA, NDOA ZA AIBU – MWAKINYO AVUNJA UKIMYA!

Image
  Bondia maarufu Hassan Mwakinyo ametikisa mitandao baada ya kutoa ujumbe mzito kwa vijana wanaokimbilia harusi za kifahari bila msingi imara wa ndoa. Katika ujumbe wake aliouachia kwenye  insta stori yake  Mwakinyo alisema: "Kabla ya kufanya harusi za vishindo na hasara chungu nzima, hakikisheni na nyie waoaji ni waume kweli mkiwa ndani. Tumechoka na hizo skendo zenu za kukosa magongo!" Ujumbe huu umeibua mjadala mkubwa mitandaoni, wengi wakikubaliana naye kuwa harusi nzuri haiwezi kufunika ndoa isiyo na misingi imara. Mwakinyo anaonekana kuwakumbusha vijana kuwa kuoa si fashion show  ni maisha halisi yanayohitaji uhalisia na uimara wa tabia. Je, wewe unasemaje kuhusu kauli hii ya Mwakinyo? Unakubaliana naye? Tupia maoni yako hapa chini! 👇

YANGA KUMRUDISHA INONGA BAKA JANGWANI

Image
  "Yanga inauhitaji mkubwa wa kusajili mchezaji wa eneo hilo, Ila kuhusu nani anakujani mapema kuzungumza kwa sasa, Lakini mchakato unaendeleana majina ya wachezaji wanatazamwa kwaajili ya kuongeza nguvu eneo hilo tumekuwa tukilifanyia kazi. Kwamuda sasa yapo mezani na tayari yameanza kufanyiwa mchakato jinala Inonga ni miongoni mwao," alisema mtoa taarifa ambaye hakutaka kutajwa jina lake. Klabu ya Yanga SC imeanza mchakato wa kusajili wachezaji wapya kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi chao, huku taarifa zikieleza kuwa kuna uhitaji mkubwa katika eneo fulani (ambalo halijatajwa rasmi). Akizungumza na Dengah Media TZ, mtoa taarifa wa karibu na klabu hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema: Yanga inauhitaji mkubwa wa kusajili mchezaji wa eneo hilo. Ila kuhusu nani anakuja ni mapema kusema kwa sasa, lakini mchakato unaendelea. Majina ya wachezaji tayari yapo mezani na yanafanyiwa kazi. Jina la Inonga ni miongoni mwao." Iwapo taarifa hizi zitathibitishwa, basi ...

YAW SIKI: “SIKUAMINI KURUDI KWA KRISTO MPAKA NILIPOKARIBIA KUFA”

Image
  Maisha Hubadilika kwa Sekunde Moja… Yaw Siki, msanii maarufu wa Ghana aliyegeukia kazi ya uhubiri, amesimulia jinsi ajali ya mwaka 2013 ilivyomfungua macho kuhusu imani yake ya kidini. Katika mahojiano aliyofanya na 3Music TV, alisema kuwa ingawa alikulia katika familia ya Kikristo, hakuwahi kuamini kabisa kuhusu kurudi kwa Yesu Kristo. Nilikuwa namjua Mungu kupitia Kristo, lakini haikuwa imani ya undani. Ilikuwa ni hadi nilipopata ajali mbaya ya gari, nikawa kitandani hospitalini, ndipo nilimuomba kaka yangu aniletee Biblia. Ndipo nilipoanza kumtafuta Mungu kwa moyo wangu wote," alisimulia Yaw Siki. Tangu siku hiyo, maisha yake yalibadilika. Leo hii, anatumia muda wake kuhubiri injili na kuwatia moyo watu wengi kujenga uhusiano wa kweli na Mungu kupitia maandiko. Unajifunza nini kutoka kwa Yaw Siki? Maisha yanaweza kubadilika ghafla — lakini daima kuna nafasi ya kuanza upya na kumkaribia Mungu.

MAMA LUKAMBA AMUWSHIA MOTO BABALEVO

Image
 

PRISCILLA AJOKE OJO SAFARI YA MREMBO WA NOLLYWOOD, MITINDO MAPENZI NA JUX

Image
  Priscilla Ajoke Ojo alizaliwa Machi 13, 2001, mjini Lagos, Nigeria. Ni mwigizaji wa Kinigeria, mwanamitindo, mshawishi mkubwa wa mitandao ya kijamii, na mjasiriamali anayechipukia kwa kasi. Akiwa binti wa mwigizaji maarufu wa Nollywood, Iyabo Ojo, Priscilla alizaliwa kwenye familia yenye mizizi ya sanaa na burudani, lakini amekuwa na bidii kubwa kuhakikisha anajijengea jina lake binafsi. 1. Maisha ya Awali na Elimu Akiwa amekulia Lagos, Priscilla alihudhuria shule bora za binafsi na kuonyesha uwezo mkubwa kitaaluma na kijamii. Mwaka 2017, baada ya kuhitimu shule ya sekondari, alijiunga na Chuo Kikuu cha Babcock kilichopo Ilishan-Remo, jimbo la Ogun, Nigeria, ambako alisomea shahada ya Sanaa ya Vyombo vya Habari na Maigizo. Hii ilimpa msingi imara wa kuendeleza ndoto zake katika burudani na mitandao ya kijamii. 2.Kazi na Mafanikio Priscilla alianza kuigiza akiwa na umri wa miaka 3 na alipata umaarufu mkubwa kwa nafasi yake kwenye filamu ya "Jejeloye" mwaka 2012 alipokuwa na ...

MUONEKANO WA KWANZA WA HARUSI YA PRISCILLA OJO NA JUMA JUX WAZUA GUMZO MTANDAONI

Image
  Harusi nchini Nigeria ni sherehe ya mitindo, elegance, na mavazi mengi tofauti – na harusi ya kitamaduni ya Priscilla Ojo na Juma Jux siyo tofauti! Hivyo basi, twende moja kwa moja kwenye muonekano wao wa kwanza, ukionyesha rangi ya zambarau ambayo hakika itakumbukwa. 1.Vazi la Asooke la Kupendeza la Priscilla Priscilla Ojo alitupatia muonekano wa kupendeza akiwa amevaa blouse ya mikono mirefu na sketi inayolingana, iliyoshonwa kwa asooke ya kifahari. Hata hivyo, sketi ndiyo iliyochukua jukwaa, ikiwa na mizinguko ya kupendeza inayobadilika kati ya rangi za zambarau na fuchsia. Kitambaa kilikuwa na mapambo ya mawe na mikufu, na kutoa athari ya kupendeza inayoenda na kila hatua. Alimaliza muonekano wake kwa vilemba vya asooke vya zambarau na ipele inayolingana. 2.Agbada ya Kifalme ya Juma Jux Juma Jux hakushindwa, kwani alionekana kama bwana harusi wa kifalme akiwa amevalia agbada ya asooke inayolingana na ya Priscilla. Mapambo ya machungwa na dhahabu kwenye mbele ya vazi yaliongez...

"MUME ANAWEZA KUCHEPUKA, LAKINI MKE HAPASWI"–Lege Miami!

Image
  Kauli ya msanii na "mtaalam wa mahusiano" Lege Miami imezua mjadala mkubwa baada ya kudai kuwa wanaume wana haki ya kuchepuka katika ndoa, lakini wanawake hawapaswi hata kufikiria kufanya hivyo. Kupitia video iliyosambaa mtandaoni, Lege alisema: "Mke aliyeweka password kwenye simu yake ni kahaba. Ukiona mume wako ana password, hiyo si sababu ya nawe kuweka. Kama huwezi vumilia mume anayechepuka, hujafikia kiwango cha kuwa mke wa ndoa." Kauli hiyo imezua hisia mseto mtandaoni huku wengi wakimshutumu kwa kueneza fikra za kizamani na za mfumo dume. Je, unakubaliana na Lege Miami kwamba mume anaweza kuchepuka lakini mke hapaswi? Tupia maoni yako hapa chini…

WASAFI HAKUNA HELA NJAA KALI-LUKAMBA

Image
  Kupitia insta story ya mpiga picha maaruf na msanii lukamba amemtolea povu kubwa babalevo akimwambia kuwa yeye bado hajapotea yupo  kwenye game hivyo apunguze shobo kumfatilia na yeye sio wa kwanza kutoka wasafi mbona wapo wengi tu.  Lakinia pia amedai kuwa wasafi hawana hela kama wanazo mbona hawalipi wafanyakazi wao vizuri watu wanajitoa kwa hali na mali  kutengeneza kazi nzuri ambazo mpaka leo wanajivunia nazo lakini hawalipwi vizuri.  Madensa wamefanya kazi na diamond miaka mingi lakini hawana kiti ila walivyotoka kujipambania wamefanikiwa tayari. "Imagine madensa wamehaso miaka kumi bila chochote maskin mpaka wamekimbia zao marekani mwaka mmoja washajenga wangekufa njaaa maskin papylion si juzi tu hao ujawaona ni lukamba tu staki shobo Jamani" Lakini pia lukamba akaendela kwa kusema kuwa wasafu pale hakuna hela ni njaa kali na ndo maana akaamua kuondoka ni jehanamu pale angekufa. Je hayo maneno ni ya kweli?

KESI YA NICOLE BERRY YAAHIRISHWA: UPELELEZI BADO HAUJAKAMILIKA

Image
  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni leo Aprili 14, 2025, imesikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili msanii maarufu wa filamu Joyce Mbaga (32), anayefahamika zaidi kwa jina la Nicole Berry, pamoja na mwenzake Rehema Mahanyu (31). Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 13, 2025, baada ya upande wa mashtaka kueleza kuwa upelelezi bado haujakamilika. Wakili wa Serikali, Rhoda Maingu, aliiambia Mahakama kuwa bado wanakamilisha taratibu za uchunguzi, hivyo wakaomba kesi iahirishwe. Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemalira alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha shauri hilo hadi tarehe tajwa kwa ajili ya kutajwa. Kwa mara ya kwanza, Nicole Berry na mwenzake walifikishwa mahakamani Machi 10, 2025, wakisomewa mashitaka matatu, mojawapo likiwa ni la kuongoza genge la uhalifu, kosa kubwa chini ya sheria za uhujumu uchumi. Mashitaka hayo yanadaiwa kutekelezwa kati ya Julai 2024 na Machi 2025 katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam. Mnamo Machi 17, 2025, Nicole alifanikiwa kupata dhamana...

HARMONIZE AWAALIKA MADEMU TU KUFUNGUA STUDIO NA GYM YAKE MPYA

Image
  Msanii maarufu wa Bongo Flava, Harmonize, ameendelea kupanua wigo wa biashara zake kwa kuzindua rasmi Konde Fitness & Studios, kituo kipya cha mazoezi na studio ya muziki iliyopo Bungeni, Dodoma.Kupitia Insta Story yake, Harmonize alishiriki video akisema,  "ITS SO EXPENSIVE TO SEE ME AROUND !!! LETS MAKE MEMORIES WEN WE MEET COZ I HAVE ALMOST EVERYTHING, I'M ONLY MISSING A HOSPITAL :MAYBE 😅😂" Harmonize katika video aliyopost insta story ametoa mialiko kwa watu kuja kuzindua studio yake pamoja gym, lakini mialiko hiyo katoa kwa wanawake tu peke yake sijui ni kweli anamaanisha au utani tu. Hii ni hatua nyingine muhimu katika safari ya Harmonize ya kujenga chapa ya Konde Gang kama zaidi ya lebo ya muziki, bali pia kama jukwaa la kukuza afya, vipaji, na biashara. Hongera kubwa ziende kwa wasanii  sasahivi wanajitahidi kuwekeza katika sehemu mbalimbali ili kujipatia kipato sasahivi na badae maana kuna maisha baada ya muziki.

USIYOYAJUA KUHUSU MWIGIZAJI CARINA

Image
  Safari ya Maisha ya Mwigizaji Hawa Hussein Ibrahim (Carina): Kutoka Skrini Hadi Mapambano ya Kiafya #RIPPearl #CarinaTheActress Hawa Hussein Ibrahim, aliyefahamika sana kwa jina lake la kisanii Carina, alikuwa mwigizaji mashuhuri wa filamu za Kibongo nchini Tanzania. Alijipatia umaarufu kupitia uigizaji wake katika filamu mbalimbali zilizopendwa na watazamaji wengi. #BongoMovies #Tanzania Mbali na uigizaji, Carina pia alionyesha kipaji chake katika tasnia ya muziki alipoonekana kama video vixen katika video ya wimbo "Oyoyo" wa msanii Bob Junior, takriban miaka minane iliyopita. Uigizaji wake mahiri katika video hiyo ulimtambulisha kwa watazamaji wengi zaidi na kuongeza umaarufu wake. #VideoVixen #BobJunior #Oyoyo Kwa bahati mbaya, katika kipindi cha miaka tisa iliyopita, Carina alikumbana na changamoto kubwa ya kiafya, akisumbuliwa na tatizo la tumbo lililohitaji kufanyiwa upasuaji mara kadhaa, jumla ya mara 24. Kutokana na hali yake, alihitaji matibabu ya hali ya juu zaidi...

FEITOTO ANARUDI YANGA

Image
         Feisal Salum 'Fei Toto' Arejea Yanga SC,                                Mashabiki Wafurahia Kiungo mshambuliaji mahiri, Feisal Salum 'Fei Toto', anarudi kwenye klabu yake ya zamani, Yanga SC, baada ya kukosekana kwa muda. Habari hizi zimewafurahisha sana mashabiki wa Yanga SC, ambao wanamtambua Fei Toto kama mchezaji muhimu kwenye timu yao. Ujumbe uliochapishwa kwenye ukurasa wa Instagram wa @feisal194 unasema: "Faila Suhfi Is Coming Back Where Is Supposed To Be." Ujumbe huu unaonyesha wazi kuwa Fei Toto anarudi kwenye klabu ambayo anahisi ni nyumbani kwake. Picha iliyoambatanishwa kwenye ujumbe huo inaonyesha Fei Toto akiwa amevaa jezi ya Yanga SC, ikiashiria kuwa amerudi rasmi kuitumikia klabu hiKurejea kwa Fei Toto kunatarajiwa kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Yanga SC, ambacho kinajiandaa kwa michezo mbalimbali ya ligi na mashindano mengine yote..

AR​​SENAL YAPATA NGUVU MPYA KABLA YA KUUMANA NA REAL MADRID: PARTEY NA WHITE WAREJEA MAZOEZINI

Image
  Arsenal Yapata Nguvu Kabla ya Vita na Real Madrid UCL! Partey na White Warejea Mazoezini Mashabiki wa Arsenal wanaweza kupumua kwa utulivu! Kuelekea mchezo wao muhimu wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid siku ya Jumatano, meneja Mikel Arteta amepokea habari njema kuhusu majeruhi. Kiungo muhimu Thomas Partey na beki imara Ben White wameonekana wakifanya mazoezi siku ya Jumanne, ikiashiria kuwa wanaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri kwenda Uhispania. Partey alilazimika kutolewa nje katika mchezo wa sare dhidi ya Brentford mwishoni mwa wiki, huku White akikosa kabisa mchezo huo kutokana na matatizo madogo ya goti. Kurejea kwao ni ongezeko kubwa la nguvu kwa Arteta, ambaye anajiandaa kwa mchezo mgumu dhidi ya mabingwa hao wa kihispania. Hata hivyo  si habari njema kwa wote, kwani Riccardo Calafiori hakuonekana kwenye mazoezi na kikosi kilichobaki. Arsenal wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na faida ya goli 3-0 waliyoipata katika mchezo wa...

YANGASC YAITANDIKA STAND UNITED 8-1, KIBABAGE NA CHAMA WAFUNGA MAGOLI YA KUFURAHISHA

Image
  Timu ya Yanga SC imeonyesha kiwango cha hali ya juu kwa kuishinda Stand United kwa magoli 8-1 katika mechi iliyopigwa hivi karibuni. Ushindi huu umewafurahisha mashabiki wa Yanga SC na kuonyesha ubora wa timu hiyo.  * Magoli Mengi: Yanga SC imefunga magoli 8, huku Stand United wakipata goli 1 pekee.  * Wafungaji: Kibabage amefunga magoli 2, Aziz Ki amefunga magoli 3, na Chama amefunga magoli 2. Musonda pia amefunga goli 1.  * Ushindi Mkubwa: Ushindi huu ni mkubwa na unaonyesha ubora wa Yanga SC. hivyo yanga ataendelea hatua inayofuta katika kombe hilo la FA.

AIBU TUPU! HASSAN MWAKINYO JR ATAJA 'USHAMBA' WA MITANDAONI KWENYE MISIBA.

Image
  Hassan Mwakinyo Jr Akemea Matumizi ya Misiba Kama Maudhui Mtandaonii Katika ujumbe wake kwenye Instagram, Hassan Mwakinyo Jr ametoa maoni yake kuhusu tabia ya baadhi ya watu kutumia misiba kama maudhui ya mitandao ya kijamii. Amesisitiza kuwa msiba ni tukio la huzuni na sio burudani, na amewataka watu kuacha "ushamba" wa kuchapisha kila kitu mtandaoni. "Wote tunafahamu kuwa msiba sio kitu cha kufurahisha ndio maana inakuwa ni siku ya majonzi. Mfiwa anapataje nguvu ya kuposti au kuandika andika IG, how unaweza kufanya msiba wako kuwa content ya msiba wa taifa guys mbona mnakuwa washamba washamba sana," aliandika Hassan Mwakinyo Jr. Jamsni tuache matumizi ya misiba kama njia ya kupata umaarufu au kujipatia maoni mtandaoni. Hassan Mwakinyo Jr anasisitiza umuhimu wa kuheshimu misiba na kuacha "ushamba" wa mitandaoni. Je ni sahihi kufanya msiba kuwa content? Dondosha comment yako apo chini

"NILIMPENDA KWA MOYO WOTE, SIJUI NI NINI KILIMVUTA KWAKO" – SAID SAID

Image
 Katika ulimwengu wa mapenzi, kila mtu ana hadithi yake ya maumivu. Post hii ya mtandaoni iliyowekwa na @saidsaid._ imegusa nyoyo za wengi, ikionyesha upande wa pili wa upendo – ule wa kuumia kimya kimya. Nishamuita majina kibaooo, wangu wa roho, kipenzi wa moyo... Sijui ni nini kafata kwako,” anaanza kwa sauti ya huzuni. Anaendelea kumkana aliyesambaza uongo juu ya mapenzi yake: Kama kakwambia nlikua simpendi – muongo. Nlikua smtoi out – muongo. Et hali hashibi – muongo. Mara nilimcheat – muongo... Ni maumivu ya moyo yanayotamka kwa mistari rahisi lakini yenye uzito mkubwa. Katika dunia ya mapenzi ya sasa, mtu anaweza kutoa kila kitu – lakini bado apoteze kila kitu. Je, umewahi kuumizwa kiasi hiki?

Muziki au Ulaghai? Peter Amchana Jude wa P-Square kwa Kutafuna N1.38bn

Image
  Bifu la kifamilia ndani ya kundi maarufu la P-Square lafika mahakamani! Peter Okoye amesimama mahakamani dhidi ya kaka yake mkubwa, Jude Okoye aliyewahi kuwa meneja wao akituhumu kutafuna zaidi ya Naira bilioni 1.38 kupitia kampuni ya Northside Music Limited Kwa mujibu wa EFCC, Jude alihusishwa na ununuzi wa jumba la kifahari Parkview Estate kwa ₦850 milioni kwa kutumia fedha zisizofahamika chanzo chake. Peter alieleza kuwa Jude alikuwa msimamizi pekee wa akaunti za kundi hilo na hakuwahi kuruhusu uwazi kwenye mapato ya kazi zao, hali iliyomlazimu kuingilia kwa msaada wa kisheria kutoka kwa Festus Keyamo. Je, hii ni kashfa ya kifedha au ni kulipizana kisasi cha kifamilia?

HELA NDIO LUGHA YA MAPENZI KW A SASA

Image
  MAPENZI BILA PESA? BADO KUNA VIJANA WANAAMINI HIVYO? Nashangaa bado kuna vijana wanaoamini kwamba mapenzi ni tofauti na pesa, wakati hali halisi inaonyesha vinginevyo. Hebu angalieni drama ya sasa mitandaoni—Zuchu na Rita wanamgombania Diamond Platnumz. Sababu si nyingine ila ni pesa na umaarufu alionao.Hebu tukumbuke historia. Diamond alivyopenda sana Wema Sepetu si kwa sababu ya sura tu, bali Wema alimkubali kipindi ambacho hakuwa na kitu kabisa. Leo hii, Wema bado anaonesha moyo wa tofauti. Anaweza kuwa na mwanaume hata kama hana pesa nyingi. Angalia uhusiano wake wa sasa na Whozu—si wa kifahari, lakini wa kipekee. Hii ni dalili ya mwanamke mwenye mapenzi ya kweli. Turudi miaka 15 nyuma, enzi za nyimbo kama Nitarejea na Mbagala. Je, Zuchu au Rita wangemgombania Diamond wakati huo? Jibu ni HAPANA. Hakuwa na hela wala umaarufu, hakuwa kivutio kwa mtu yeyote isipokuwa kwa wale waliompenda kwa moyo wa kweli. Leo wanamgombania kwa sababu ya PESA. Madhara ya wanawake kufuata wanaume...

HATIMAYE MAMA YAKE MEJA KUNTA APYMZISHWA KATIKA NYUMVA YAKE YA MILELE

Image
  Mwili wa mama mzazi wa msanii wa singeli meja kunta umezikwa katika makaburi ya tandika dar es salaam siku ya leo baada ya kifo kutokea jana ambapo mama ake meja kunta alianguka ghafla. Watu wengi kutoka taasisi mbalimbali walijitokeza lakini wasanii pia walijitokeza kummunga na kumpa pole msanii mwenzao Mrja kunja kwa kipindi hiki kigumu anachopitia.

WACHEZAJI WA REAL MADRID WATOA ONYO KALI

Image
  Baada ya kichapo kizito cha mabao 3-0 kutoka kwa Arsenal katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid wameonyesha wazi kuwa hawajakata tamaa. Mchezo wa marudiano unatarajiwa kupigwa Jumatano hii kwenye dimba la Santiago Bernabéu, na tayari nyota wa Real Madrid wametuma ujumbe mzito kwa Arsenal kupitia mitandao ya kijamii. Jude Bellingham, mmoja wa wachezaji wa kutegemewa msimu huu, alichapisha kwenye ukurasa wake: “Tutaonana Jumatano, Madridistas!” – ujumbe mfupi lakini uliojaa maana kwa mashabiki wa Los Blancos. Vinicius Junior naye hakuachwa nyuma. Akiwa na beji ya nahodha, aliandika: “Tayari nafikiria kuhusu Jumatano!!! Tuko tayari na tunaisubiri kwa hamu. Tutawangoja Bernabéu na tutapambana hadi mwisho. SISI NDIO REAL!!! HALA MADRID!” Rodrygo alimalizia kwa kusema: “Tutaonana Jumatano, Madridistas! Nyinyi ni muhimu sana! TWENDE MADRID!” Kwa upande wa Arsenal, walitawala mchezo wa kwanza kwa mabao kutoka kwa Declan Rice na Mikel Merino, wakiji...

Meja Kunta Ashuhudia Mwili wa Mama Yake kwa Mara ya Kwanza, Aeleza Uchungu

Image
  Msanii wa Bongo Fleva, Meja Kunta, amefunguka kuhusu uchungu anaoupitia baada ya kumpoteza mama yake mzazi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Meja Kunta alishiriki ujumbe mzito akielezea jinsi alivyoshuhudia mwili wa mama yake kwa mara ya kwanza. "Leo kwa mara ya kwanza na shuhudia mwili wa marehemu kwa mara ya kwanza alafu ni mama yangu," aliandika Meja Kunta, akionyesha uchungu mkubwa aliokuwa nao. Ujumbe huo unaelezea wazi jinsi msanii huyo alivyoguswa na msiba huo na jinsi ilivyokuwa vigumu kwake kuona mwili wa mama yake. Mashabiki na wafuasi wa Meja Kunta wameendelea kumtumia salamu za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii, wakimuunga mkono katika kipindi hiki kigumu. Wengi wao wamempa pole na kumtia moyo, wakimtakia nguvu na uvumilivu. Tunaungana na Meja Kunta katika kipindi hiki cha majonzi na tunatoa pole zetu za dhati kwa familia na marafiki. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema pepomi. Lakini msanii meja kunta ametoa taarufa ya mazishi yatafayika Dar es sal...

SALAH AWEKA REKODI MPYA YA MCHANGO WA MABAO KATIKA PREMIER LEAGUE

Image
 Mohamed Salah aliweka historia katika Premier League siku ya Jumapili baada ya kufikisha jumla ya mchango wa mabao 45 msimu huu—akiivunja rekodi ya awali ya 44 iliyokuwa inashikiliwa kwa pamoja na Thierry Henry (2002–03) na Erling Haaland (2022–23). Katika ushindi wa Liverpool wa 2-1 dhidi ya West Ham huko Anfield, Salah alitoa pasi murua ya trivela iliyomuwezesha Luis Díaz kufunga bao katika kipindi cha kwanza. Hii ilikuwa asisti yake ya 18 msimu huu, na anashikilia nafasi ya kwanza kwa idadi ya asisti katika ligi. Tayari pia ana mabao 27 katika msimu huu wa Premier League. Kwa kasi aliyonayo, Salah sasa yuko njiani kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya msimu mmoja wa mechi 38 wa Premier League kufikisha au kuvuka jumla ya michango 50 ya mabao—hii ni rekodi ya kipekee kwa nyota huyu wa Misri.

MEJA KUNTA AMPOTEZA MAMA YAKE MZAZI

Image
  Msanii wa muziki wa singeli, Meja Kunta, amepata pigo kubwa baada ya kumpoteza mama yake mzazi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Meja Kunta alishiriki picha yenye ujumbe mzito, "RIP Mom," ikiambatana na picha ya mshumaa unaowaka, kuashiria huzuni yake. Picha hiyo pia ina maneno "Rest In Peace," yanayoonesha masikitiko yake na kumuombea mama yake apumzike kwa amani. Ujumbe huo mfupi lakini wenye hisia kali unaelezea wazi jinsi msanii huyo alivyoguswa na msiba huo. Mashabiki na wafuasi wa Meja Kunta wamekuwa wakimtumia salamu za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii, wakimuunga mkono katika kipindi hiki kigumu. Wengi wao wamempa pole na kumtia moyo, wakimtakia nguvu na uvumilivu. Tunaungana na Meja Kunta katika kipindi hiki cha majonzi na tunatoa pole zetu za dhati kwa familia na marafiki. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

ENG. HERSI SAID APATA TUZO YA KIMATAIFA KUTOKA WORLD FOOTBALL SUMMIT (WFS)

Image
  Rais wa Klabu yetu na Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu Afrika (Africa Clubs Association - ACA), Mhandisi Hersi Said, ametunukiwa tuzo maalum kutoka World Football Summit (WFS) kama kutambua mchango wake mkubwa katika kuunganisha na kuendeleza ushirikiano baina ya vilabu vya soka barani Afrika. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa soka – WFS, uliofanyika katika Jiji la Rabat, nchini Morocco Kupitia nafasi yake kama Mwenyekiti wa ACA, Eng. Hersi amekuwa mstari wa mbele kusukuma ajenda ya maendeleo ya vilabu vya Afrika, ushirikiano wa kiufundi, biashara ya soka, na uwezeshaji wa vipaji kupitia jukwaa la umoja huo. Tunampongeza kwa heshima hii kubwa ya kimataifa — ni ushindi si kwake binafsi tu, bali kwa klabu yetu, nchi na bara la Afrika kwa ujumla

SIDHANI KAMA NI HAKI KUOA MKE MMOJA-RMD

Image
  Mwigizaji maarufu wa Nollywood, Richard Mofe-Damijo (RMD), amezua gumzo mitandaoni baada ya kutoa maoni yake kuhusu ndoa ya wake wengi. Katika mahojiano ya hivi karibuni kwenye kipindi cha Curiosity Made Me Ask, RMD alieleza kuwa haoni haki mwanaume kuoa mke mmoja tu, hasa ikizingatiwa kuwa kuna wanawake wengi wanaomtamani. Mtangazaji wa kipindi hicho, Bae U Barbie, alimuuliza, “Umeoa mke mmoja tu. Je, unadhani hilo ni haki? Je, una wazo la ni wanawake wangapi wanakutamani?” Kwa majibu ya kushangaza, RMD alisema: “Sina wazo, lakini nadhani si haki kuoa mke mmoja tu. Baba yangu alikuwa na wake watano.” Kauli hiyo imeibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wake, huku wengine wakimuunga mkono na wengine kupinga vikali. Kwa sasa, RMD ameoa mtangazaji wa televisheni Jumobi Adegbesan, ambaye walifunga ndoa naye baada ya kumpoteza mke wake wa kwanza, May Ellen ‘MEE’ Mofe-Damijo, aliyefariki mwaka 1996 Je, wewe unasemaje kuhusu maoni ya RMD? Je, ndoa ya wake wengi ni haki au ni kinyum...

MAUA SAMA KUVUNJA REKODI YAKE MWENYEWE

Image
  Baada ya IOKOTE kuacha alama isiyofutika kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Flava, msanii mahiri Maua Sama ameibuka na kauli ya kusisimua inayozidi kuwasha moto wa matarajio kwa mashabiki wake: "Wimbo wangu wa IOKOTE uliweka historia kubwa sana... Lakini my next release inaenda kuvunja rekodi ya IOKOTE – I PROMISE YOU!" Kauli hiyo imekuwa gumzo mitandaoni, ikionesha jinsi Maua Sama alivyo na imani na kazi anayokuja nayo. Ikiwa IOKOTE ilikuwa ni mlipuko wa ubunifu na miondoko ya kipekee, basi ni wazi kuwa kuna jambo kubwa linakuja. Mashabiki sasa wanabaki na maswali: Je, wimbo huu mpya ni collabo au solo? Je, anazungumzia mapenzi, nguvu ya mwanamke, au maisha kwa ujumla? Na je, ataachia lini? Kwa sasa, kila mtu ana macho kwa Maua Sama, akisubiri kwa hamu wimbo huo mpya kuvunja rekodi nyingine tena!

Hesabu za Kibu Denis Kuwa Mfungaji Bora CAF ziko Hivi....

Image
  Anaandika ✍️ @cheyolutenganotz Kibu Denis anaisaka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa michuano ya kombe la shirikisho ikiwa anahitaji goli 2 kwenye mchezo ujao ili kumfikia kinara wa sasa. Ismail Belkacemi kutoka Usm Alger ndiye anaongoza akiwa tayari amefunga magoli 5 moja likiwa kwa mkwaju wa penalti. Ismail tayari ameondoshwa na timu yake hivyo hana uwezo wa kuongeza goli nyingine za ziada Anayeshika nafasi ya pili ana magoli manne (4) Ifeanyi Ihemekwele wa Enyimba United ambaye pia aliyolewa kwenye michuano. Kibu Denis ana nafasi kubwa ya kuwa kinara ukizingatia factor zifuatazo........ Waliopo juu yake wote wameondolewa kwenye michuano hivyo kazi kwake ni kufunga pekee. Kibu Denis anakutana Stellenbosch ambao safu yao ya ulinzi inavuja kwa kiasi kikubwa imeruhusu mabao 10 kwenye hatua ya makundi yenye mechi 6 pekee Kwenye ligi wameruhusu magoli 17 katika michezo 20 na kenda. Kibu anaweza kufunga nyumbani na ugenini kwa kuwa tayari ameonyesha kiwango bora hata mechi za ugenini r...

CHELSEA WAWINDA VIJANA HATARI KUTOKA LA LIGA NA PREMIER LEAGUE!

Image
  Klabu ya Chelsea imeweka jicho kwa beki chipukizi Dean Huijsen (19), anayekipiga Bournemouth kwa sasa. Hata hivyo, The Blues wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa vilabu vingine vya Ligi Kuu ya England vinavyotaka huduma yake. Wakati huohuo, Chelsea pia wanahusishwa na winga wa kasi kutoka Real Betis, Jesus Rodriguez (19), ambaye ana kipengele cha kuachwa kwa dau la hadi £42 milioni. Je, vijana hawa wataingia rasmi Stamford Bridge msimu ujao? Endelea kufuatilia Dengah Media TZ kwa taarifa motomoto za usajili!

FIREBOY DML: “BABA YANGU HATANISAMEHE KWA TATOO NILIZOCHORA”

Image
  Msanii maarufu wa muziki kutoka Nigeria, Adedamola Adefolahan, anayefahamika zaidi kwa jina la kisanii Fireboy DML, amefunguka kuhusu mgongano wa kimtazamo uliopo kati yake na baba yake kuhusu masuala ya tatoo. Akiwa mgeni katika kipindi cha 90s Baby Show, Fireboy alisema kuwa moja ya mambo yanayoumiza moyo wa baba yake ni tatoo alizojiwekea mwilini. “Jambo moja ambalo linaweza kumvunja baba yangu moyo? Nafikiri tayari nimeshafanya – tatoo zangu. Kila anapokuja kunitembelea, huwa nimevaa jalabiya, nimejifunika kabisa. Kwa sababu tatoo, humuumiza moyo kila mara anapoziona,” alisema Fireboy. Ingawa baba yake hana tatizo na hereni alizochoma, msanii huyo alisisitiza kuwa tatoo ni jambo ambalo baba yake hawezi kulikubali kamwe. “Baba yangu hana shida na hereni, lakini hizi tatoo? Hatanisamehe kamwe kwa vitu hivi,” aliongeza. Fireboy alifafanua kuwa mapenzi yake kwa tatoo hayawezi kuhusishwa tu na kazi yake ya muziki. Alisema hata kama angekuwa na taaluma ya kawaida kama ya benki, bad...

ZENDAYA NA TOM HOLLAND WAPANGA HARUSI YA KIFAHARI MWAKA 2026!

Image
  Mtaalamu maarufu wa mitindo, Law Roach, amethibitisha kuwa atahusika moja kwa moja katika maandalizi ya harusi ya nyota wawili wa Hollywood, Zendaya na Tom Holland. Hii ni baada ya Zendaya kuonekana akiwa na pete ya almasi yenye uzito wa gramu moja kwenye hafla ya tuzo za Golden Globes 2025, ishara ya kuthibitisha uchumba wao Akizungumza katika hafla ya Fashion Trust Awards jijini Los Angeles, Law Roach alisema: "Harusi bado ipo mbali… wote wana miradi mingi ya filamu mwaka huu na matukio mengi mwaka ujao. Mimi napumzika kwa ajili ya 2026" Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa mapema na baba wa Tom Holland, Dominic Holland, Tom alimposa Zendaya kwa njia ya kipekee, kwa maandalizi makini na ya faragha. Kupitia akaunti yake ya Patreon, Dominic aliandika: "Alinunua pete, akaomba ruhusa kwa baba wa Zendaya, na alipanga kila kitu – wakati, mahali, maneno ya kusema na hata mavazi." Wawili hao si tu wanapanga ndoa, bali pia wanatarajiwa kushirikiana tena katika kazi kubwa z...

FIREBOY DML, KUTOKA KUUZA SUPU YA NYAMA MTAANI MPAKA KUWA MSANII MKBUWA AFRIKA

Image
Adedamola Adefolahan, maarufu kama Fireboy DML, ni mmoja wa wasanii maarufu wa muziki wa Afrobeats kutoka Nigeria. Lakini kabla ya kuwa jina kubwa katika muziki, Fireboy alikuwa akijiandaa kuanza maisha ya biashara ya kujikimu. Hadithi yake ni ya kuvutia na inatoa matumaini kwa watu wengi wanaopambana na changamoto za maisha. Katika mahojiano ya hivi karibuni kwenye kipindi cha 90s Baby Show kilichofanyika  London, Fireboy alifunguka kuhusu safari yake ya kutafuta mafanikio. Alieleza jinsi alivyokuwa karibu kuanza biashara ya kuuza taa za kuchaji chini ya Daraja la Ajah, Lagos, baada ya kutafuta njia ya kujikimu. Alikubaliana na mtu mmoja ambaye alimuonyesha jinsi ya kufanya biashara hiyo, lakini kwa wakati huo, alijua kuwa hiyo siyo njia yake ya kufika mbali. Nilikuwa nikizingatia kuuza taa za kuchaji. Nilikutana na mtu mmoja chini ya Daraja la Ajah, alikuwa akinieleza kuhusu biashara hiyo, na nikamwambia nilikuwa na nia," Fireboy alieleza. Wakati huo, Fireboy alikuwa pia anauza ...

ALICHOKIFANYA DULLA MAKABILA BAADA YA NDOA YA MANARA NA ZAIYLISSA KUVUNJIKA

Image
  Dulla makabila ameonesha kufurahi baada ya ndoa ya manara na zayissa kuvunjika na hii ndo ilikuwa reaction yake.

HAJI MANARA NA ZAIYLISSA WAMEACHANA RASMI: HALI YA NDOA YAO YAVUNJIKA

Image
  Habari mpya kutoka kwa mrembo Zaiylissa na mchumba wake Haji Manara zimevuta hisia za wengi mitandaoni. Inaripotiwa kuwa, jana Aprili 9, 2025, wawili hao walitangaza rasmi kwamba wameachana baada ya kipindi cha ndoa ambayo imekuwa na misukosuko kadhaa. Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika, Haji Manara amethibitisha kuachana na Zaiylissa kwa kutoa talaka tatu, akisema kuwa walijaribu kuokoa ndoa yao lakini walishindwa kufika kwenye muafaka. "Mambo yalikuwa magumu na hatukuweza kuendelea kwa pamoja," alisema Manara katika taarifa aliyoitoa. ●Misukosuko ya Ndoa Katika miezi ya hivi karibuni, kulikuwa na uvumi kwamba ndoa yao ilikuwa na matatizo, lakini wawili hao walikuwa wakijitahidi kuziba pengo hilo kwa kupost picha na video za pamoja mitandaoni. Hata hivyo, baadhi ya mashabiki waligundua kuwa Zaiylissa alikuwa akitokea kutoonekana kwenye matukio mengi yaliyohusisha familia ya Manara, jambo ambalo liliongeza hisia za kutokea kwa mgogoro. ●Zaiylissa aeleza Kilichotokea Akizung...

IJUE HISTORIA YA KUVUTIA YA KLABU YA STELLENBOSCH – KUTOKA KUSIKOJULIKANA HADI KUANGAZA AFRIKA!

Image
  1. Historia ya Klabu ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini Stellenbosch Football Club ni moja kati ya vilabu vinavyokua kwa kasi kwenye soka la Afrika Kusini. Kikiwa kinatokea mjini Stellenbosch, katika Jimbo la Western Cape, klabu hii imejipatia umaarufu mkubwa kwa muda mfupi kutokana na uongozi bora, sera nzuri za kukuza vipaji, na mtindo wa kipekee wa uchezaji. 2.Mwanzo wa Safari Stellenbosch FC ilianzishwa rasmi mwaka 2016 baada ya kampuni ya Stellenbosch Academy of Sport (SAS) kuinunua timu ya Vasco da Gama FC iliyokuwa ikicheza kwenye ligi daraja la kwanza (National First Division). Baada ya ununuzi huo, jina la timu lilibadilishwa kuwa Stellenbosch FC, na lengo kuu likawa ni kuikuza timu hiyo hadi kufikia Ligi Kuu ya Afrika Kusini (Premier Soccer League – PSL). 3. Kuelekea Ligi Kuu Stellenbosch FC ilipanda daraja hadi PSL msimu wa 2018/2019 baada ya kumaliza ligi ya daraja la kwanza ikiwa kinara. Ilikua ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kushiriki kwenye ligi ya juu zaidi nchin...

WIZI MKUBWA WA BENKI NCHINI AFRIKA KUSINI

Image
    Mwaka 2014, Afrika Kusini ilishuhudia mojawapo ya wizi mkubwa, wa kushangaza, na uliopangwa kwa ustadi mkubwa kuwahi kutokea katika historia ya taifa hilo. Lengo kuu lilikuwa benki ya First National Bank (FNB) iliyoko Randburg, Johannesburg. Kiasi kilichoibiwa? Zaidi ya R50 milioni (takriban dola milioni 3.5 za Kimarekani). Huu haukuwa wizi wa kawaida – ulikuwa ni maonyesho ya ustadi wa kupanga, subira ya hali ya juu, na uelewa wa ndani wa mifumo ya benki. MAANDALIZI YA MIPANGO YAO Wahalifu hawakuvamia benki kwa bunduki. Walikuwa werevu zaidi. Kwanza kabisa, walikodisha duka dogo karibu kabisa na benki hiyo, wakijifanya ni wafanyabiashara wa kawaida. Kutokea hapo, walitumia miezi kadhaa wakichimba handaki la siri lililowaongoza moja kwa moja hadi chini ya benki, kwenye chumba cha kuhifadhia fedha (vault). Kazi ya kuchimba handaki ilifanywa usiku tu, kwa utulivu mkubwa ili kuepuka kusikika kwa kelele. Inaaminika walikuwa na vifaa vya kitaalamu na huenda walisaidiwa na wataa...

WABABE WA SIMBA WAMEWASILI DAR ES SALAAM KUMALIZA SHUGHULI YAO

Image
  Kikosi cha Al Masry 🇪🇬 kimewasili jijini Dar Es Salaam 🇹🇿 tayari kwa mechi yao ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya wenyeji Simba Sc itakayopigwa Aprili 9 katika uwanja wa Benjamin Mkapa. Ikumbukwe mechi ya mkondo wa kwanza simba alipata kichapo cha mabao mawili kwa bila ugenini hivyo simba anatakiwa kushinda nyumbani kwake mabao kuanzia mawili ili kujihakikishia tiketi ya kufuzu nusu fainali kombe la shirikisho barani afrika.

Ni LAZIMA UFANYE KAZI HARAMU ILI UPATE MAFANIKIO

Image
  Muigizaji na mtayarishaji maarufu wa Nigeria, Funke Akindele, amesema ili mtu yeyote afanikiwe na kufanya makubwa maishani ni lazima mtu awe tayari kufanya kazi (haramu) chafu. Akiongea kwenye podcast ya 'WithChude', Akindele alieleza kuwa kufanya kazi hiyo chafu ni moja ya hitaji la kupata mafanikio katika taaluma yake. Kwa kuongezea, mwigizaji huyo aligundua bidii na kujitolea kwa kazi na majukumu kama ufunguo wa mafanikio. Akifichua siri za mafanikio yake ambayo yalikuwa yanazungumzwa zaidi, Akindele alisema, "Niseme kwamba watu wengi wanataka kufanya ninachofanya, lakini ninaendelea kuwaambia: ili ufanikiwe, unahitaji kufanya kazi kwa bidii na kufanya kazi chafu (Haramu)". Alishikilia kuwa alikataa kukaa juu au kuruhusu mafanikio ya sasa katika tasnia kuathiri kazi yake, lakini alibakia kulenga na bila kukengeushwa. Ingawa hakuondoa nafasi ya kiroho katika safari ya burudani, aliangazia umuhimu wa kujitambua na uhalisi katika kupiga hatua katika sekta hiyo, akih...

MAJUKUMU YANAWEZA KUMFANYA MUME AKAKOSA MAPENZI NA MKE WAKE

Image
  Mwangalizi Mkuu wa Jiji la Potter, Nabii Nanasei Opoku-Sarkodie, amesema kuwa majukumu mengi yanayoletwa na ndoa yanaweza kushawishi mwanamume kutokuwa na mapenzi na mke wake. Nabii alisema, wanaume wengi walio kwenye ndoa hujishughulisha na kutekeleza majukumu yao ya nyumbani, kama vile kuwalipia watoto wao karo ya shule na kuwagharamia kila siku, jambo ambalo linaweza kuwaelemea. Kwa sababu hiyo, baadhi ya wanaume wanaweza kukosa muda au nguvu za kushiriki katika shughuli za kimapenzi kama vile kumbusu, kukumbatiana, au ishara nyingine ambazo wake zao wanaweza kutamani. Nabii Opoku-Sarkodie alishauri dhidi ya kuchagua mchumba kwa kuzingatia sura ya kimwili tu, akisisitiza umuhimu wa subira na kuvumiliana katika kudumisha ndoa. "Majukumu yanaweza kumfanya mumeo asiwe na mapenzi, lakini hiyo haimaanishi kuwa hakupendi. Amejikita katika kulipa bili na kutimiza majukumu mengine. Kuna mambo nilikuwa nafanya ambayo sifanyi tena kwa ufahamu, kama kusema, 'Oh, nipe busu, nikumbati...

MOURINHO APIGWA RUNGU MECHI TATU

Image
 Meneja wa Fenerbache, Jose Mourinho, amefungiwaa mechi tatu kwa kumbana pua kocha wa Galatasaray, Okan Buruk. Kisa hicho kilitokea baada ya vijana hao wa Mourinho kushindwa katika Kombe la Super Cup na wapinzani wao. Kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Manchester United alikwenda nyuma ya Buruk na kushika pua yake, kisha kumsukuma chini kocha mwenzie. Inaaminika Shirikisho la Soka la Uturuki lilichunguza uwezekano wa kumfungia mechi tano hadi 10 Mourinho, lakini wakachagua kupunguza adhabu yake baada ya kukubali kwamba hapo awali alichokozwa na Buruk muda wote. Hii ni mara ya pili mwaka wa 2025 kwa Mourinho kufungiwa mechi kadhaa, baada ya kupigwa mechi nne mwezi Februari kwa kutoa maoni ya ubaguzi wa rangi kuhusu benchi la Galatasaray.

AZIZ KI ,MCHEZAJI ANAECHUKUA MKWANJA MREFU AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Image
 Kupitia kwenye Jarida la Africa Facts Zone limetoa orodha ya Wachezaji wanaolipwa mkunjwa mrefu zaidi kwa mwaka kwa wachezaji wanaochezea soka la ndani ya Afrika. Katika Orodha hiyo Mchezaji anayeongoza ni Raia wa Misri anayechezea klabu ya Al ahly Ali Maaloul ambaye ni beki wa Kushotoa akilipwa dola milioni 1.5 ambayo ni zaidi ya Tsh bilioni 3 kwa Mwaka. Aziz Ki kutoka klabu ya Yanga yupo nafasi ya Nne akilipwa dola laki mbili na elfu Arobani ambayo ni zaidi ya milioni 640 kwa Mwaka akiwa Yanga. Mshahara huo kwa mwaka maana yake kwa mwezi analipwa dole Elfu Ishirini ambayo ni sawa milioni 53 za Kitanzania kwa mmoja. Mukwala wa Simba nafasi ya 6 akilipwa dola $108,000 ambayo ni zaidi ya milioni 288 za Kitanzania na kwa Mwezi analipwa dola 9,000 zaidi ya Tsh milioni 24 kwa Mwezi Simba. Orodha hiyo hii hapa chini. Highest Paid Players in African Leagues Annually - 1. Egypt - Ali Maaloul | $1.5 million | Al Ahly 2. South Africa - Ronwen Williams >= | $320,000 | Mamelodi Sundowns 3...