Meja Kunta Ashuhudia Mwili wa Mama Yake kwa Mara ya Kwanza, Aeleza Uchungu
Msanii wa Bongo Fleva, Meja Kunta, amefunguka kuhusu uchungu anaoupitia baada ya kumpoteza mama yake mzazi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Meja Kunta alishiriki ujumbe mzito akielezea jinsi alivyoshuhudia mwili wa mama yake kwa mara ya kwanza.
"Leo kwa mara ya kwanza na shuhudia mwili wa marehemu kwa mara ya kwanza alafu ni mama yangu," aliandika Meja Kunta, akionyesha uchungu mkubwa aliokuwa nao. Ujumbe huo unaelezea wazi jinsi msanii huyo alivyoguswa na msiba huo na jinsi ilivyokuwa vigumu kwake kuona mwili wa mama yake.
Mashabiki na wafuasi wa Meja Kunta wameendelea kumtumia salamu za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii, wakimuunga mkono katika kipindi hiki kigumu. Wengi wao wamempa pole na kumtia moyo, wakimtakia nguvu na uvumilivu.
Tunaungana na Meja Kunta katika kipindi hiki cha majonzi na tunatoa pole zetu za dhati kwa familia na marafiki. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema pepomi.
Lakini msanii meja kunta ametoa taarufa ya mazishi yatafayika Dar es salaam Temeke Tandika Kilimahewa mida ya saa 7 kama upo karibu na maeneo hayo nenda kashiriki mazishi hayo na utapata thawabu.
Comments
Post a Comment