Muziki au Ulaghai? Peter Amchana Jude wa P-Square kwa Kutafuna N1.38bn
Bifu la kifamilia ndani ya kundi maarufu la P-Square lafika mahakamani! Peter Okoye amesimama mahakamani dhidi ya kaka yake mkubwa, Jude Okoye aliyewahi kuwa meneja wao akituhumu kutafuna zaidi ya Naira bilioni 1.38 kupitia kampuni ya Northside Music Limited
Kwa mujibu wa EFCC, Jude alihusishwa na ununuzi wa jumba la kifahari Parkview Estate kwa ₦850 milioni kwa kutumia fedha zisizofahamika chanzo chake. Peter alieleza kuwa Jude alikuwa msimamizi pekee wa akaunti za kundi hilo na hakuwahi kuruhusu uwazi kwenye mapato ya kazi zao, hali iliyomlazimu kuingilia kwa msaada wa kisheria kutoka kwa Festus Keyamo.
Je, hii ni kashfa ya kifedha au ni kulipizana kisasi cha kifamilia?
Comments
Post a Comment