HELA NDIO LUGHA YA MAPENZI KW A SASA
Nashangaa bado kuna vijana wanaoamini kwamba mapenzi ni tofauti na pesa, wakati hali halisi inaonyesha vinginevyo. Hebu angalieni drama ya sasa mitandaoni—Zuchu na Rita wanamgombania Diamond Platnumz. Sababu si nyingine ila ni pesa na umaarufu alionao.Hebu tukumbuke historia. Diamond alivyopenda sana Wema Sepetu si kwa sababu ya sura tu, bali Wema alimkubali kipindi ambacho hakuwa na kitu kabisa. Leo hii, Wema bado anaonesha moyo wa tofauti. Anaweza kuwa na mwanaume hata kama hana pesa nyingi. Angalia uhusiano wake wa sasa na Whozu—si wa kifahari, lakini wa kipekee. Hii ni dalili ya mwanamke mwenye mapenzi ya kweli.
Turudi miaka 15 nyuma, enzi za nyimbo kama Nitarejea na Mbagala. Je, Zuchu au Rita wangemgombania Diamond wakati huo? Jibu ni HAPANA. Hakuwa na hela wala umaarufu, hakuwa kivutio kwa mtu yeyote isipokuwa kwa wale waliompenda kwa moyo wa kweli. Leo wanamgombania kwa sababu ya PESA.
Madhara ya wanawake kufuata wanaume wenye fedha ni makubwa. Kwanza kabisa, mwanaume hawezi kumpenda kwa dhati mwanamke anayemfuata kwa pesa. Atakuwa naye kwa ajili ya ‘utamu’ tu, na sio mapenzi ya kweli. Ndiyo maana unaweza kuona hadi sasa katika vita yote kati ya Zuchu na Rita, Diamond hajachukua upande wowote. Hajamtetea Zuchu wala Rita, kwa sababu anajua wote wana tamaa ya mali, siyo mapenzi ya dhati.
Swali ambalo wengi hujiuliza ni: kwa nini Diamond aliwahi kumpenda sana Sarah? Jibu ni rahisi—Sarah alikubali kuwa naye kipindi cha maisha magumu, akavumilia naye hadi sasa. Lakini kwa wengine kama Mobetto, Zari, Tanasha, Zuchu, na sasa Rita, ni kama wote wana lengo moja: kuingia kwenye maisha ya Diamond kupitia njia ya mimba. Mobetto, Zari na Tanasha walishapata watoto na Diamond, na kwa sasa Rita naye aliwahi kupata ujauzito (japo ukaharibika). Zuchu bado tu hajategesha—na hilo nalo ni swali kubwa kwa wengi.
Sasa katikati ya vita ya wanawake hawa, Diamond anapost vocha ya milioni 9, na kusema amechoka na Rolls Royce yake, anaagiza Bugatti mpya. Hii ni njia yake ya kuonesha kuwa ana hela, na anajua kabisa ndicho kinachowavutia wanawake wengi wanaomzunguka.S
OMO LA LEO: Wanaume—tafuteni hela! Mkishakuwa na fedha, mtakuwa huru kwenye mahusiano yenu. Mtajua nani anakupenda kwa dhati, na nani anatafuta faida. Nani wa kumuoa, na nani wa kupita naye tu.
Tunaishi kwenye zama ambapo mapenzi yamevaa sura ya biashara. Usijidanganye—hela ndiyo lugha ya mapenzi ya sasa.
Comments
Post a Comment