JINSI NILIVYOKUTANA NA MUME WANGU JUMA JUX’ – PRISCILLA OJO
Priscilla Ojo, binti wa mwigizaji maarufu wa Nigeria Iyabo Ojo, amefunguka kuhusu jinsi alivyokutana na mume wake, msanii maarufu wa Tanzania, Juma Jux. Katika video ya mahojiano inayotrend mitandaoni, alieleza kuwa walikutana kwa mara ya kwanza kwenye safari ya kibiashara nchini Rwanda. Alisema:
Tulikutana kwenye safari ya kibiashara nchini Rwanda, aliniona kwanza kwenye daraja la biashara (business class), halafu tukakutana tena hotelini. Alinipa namba yake na kuniambia nimtume ujumbe lakini sikufanya hivyo. Lakini baadaye alijua namna ya kunifikia na tukaanza kuzungumza.”
Uhusiano wao uliendelea na hatimaye kupelekea harusi ya kitamaduni iliyofanyika Lagos, Nigeria, tarehe 17 Aprili 2025, baada ya kufunga ndoa ya Kiislamu nchini Tanzania mwezi Februari.JP2025: ‘Jinsi nilivyokutana na mume wangu Juma Jux’ – Priscilla Ojo
Harusi hiyo imekuwa gumzo kubwa mitandaoni, na baadhi ya watu wakiiita "harusi ya mwaka," huku ikilinganishwa na harusi ya msanii Davido.
Comments
Post a Comment