SIDHANI KAMA NI HAKI KUOA MKE MMOJA-RMD

 


Mwigizaji maarufu wa Nollywood, Richard Mofe-Damijo (RMD), amezua gumzo mitandaoni baada ya kutoa maoni yake kuhusu ndoa ya wake wengi.

Katika mahojiano ya hivi karibuni kwenye kipindi cha Curiosity Made Me Ask, RMD alieleza kuwa haoni haki mwanaume kuoa mke mmoja tu, hasa ikizingatiwa kuwa kuna wanawake wengi wanaomtamani.

Mtangazaji wa kipindi hicho, Bae U Barbie, alimuuliza, “Umeoa mke mmoja tu. Je, unadhani hilo ni haki? Je, una wazo la ni wanawake wangapi wanakutamani?”

Kwa majibu ya kushangaza, RMD alisema:

“Sina wazo, lakini nadhani si haki kuoa mke mmoja tu. Baba yangu alikuwa na wake watano.”

Kauli hiyo imeibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wake, huku wengine wakimuunga mkono na wengine kupinga vikali.

Kwa sasa, RMD ameoa mtangazaji wa televisheni Jumobi Adegbesan, ambaye walifunga ndoa naye baada ya kumpoteza mke wake wa kwanza, May Ellen ‘MEE’ Mofe-Damijo, aliyefariki mwaka 1996

Je, wewe unasemaje kuhusu maoni ya RMD? Je, ndoa ya wake wengi ni haki au ni kinyume na maadili ya kisasa? Tuachie maoni yako hapa chini.

Comments

Popular posts from this blog

MAJUKUMU YANAWEZA KUMFANYA MUME AKAKOSA MAPENZI NA MKE WAKE

Ni LAZIMA UFANYE KAZI HARAMU ILI UPATE MAFANIKIO