PAPAYA EX AZUA TAHARUKI KWENYE HARUSI YA PRISCILLA OJO – AVAA VAZI LENYE PICHA YA BWANA HARUSI KIFUANI

 



Katika harusi ya kifahari iliyofanyika Lagos, Nigeria tarehe 17 Machi 2025, Priscilla Ojo – mwana wa muigizaji mashuhuri Iyabo Ojo – alifunga ndoa ya kitamaduni na mpenzi wake kutoka Tanzania, Juma Jux. Tukio hilo lilihudhuriwa na mastaa wengi wa Afrika, lakini lililowashangaza wengi zaidi ni tukio la Papaya Ex, mrembo maarufu na mjasiriamali wa mitandaoni.

Papaya Ex alitinga harusini akiwa amevaa vazi lenye picha ya Juma Jux (bwana harusi) kifuani, na picha ya Priscilla (bibi harusi) kiunoni. Wakati wa sherehe, alitoka na kuanza kumwagia maharusi pesa huku vazi lake likiwa wazi kabisa kwa kila mtu kuona.

Hali hiyo ilimkasirisha Priscilla ambaye alimkabili kwa swali, “Kwa nini umeweka picha ya mume wangu kifuani?” Papaya Ex alimjibu kwa utulivu, “Samahani baby, ni kwa sababu nakupenda.”

Baadaye alieleza kuwa alifanya hivyo kwa ajili ya kupata attention mitandaoni.

Harusi hiyo ilihudhuriwa na mastaa kama Diamond Platnumz, Mercy Aigbe, Peter Okoye, Ebenezer Obey, Femi Adebayo, na wengine wengi.

Video ya tukio hilo inazidi kusambaa mitandaoni huku watu wakijadili kama hilo lilikuwa kiki au kutoheshimu ndoa ya watu.


Tazama video hapa:👇

https://www.instagram.com/reel/DIkScKLMpFX/?igsh=MTJoNjdvbWdqOGVubQ==

Comments

Popular posts from this blog

MAJUKUMU YANAWEZA KUMFANYA MUME AKAKOSA MAPENZI NA MKE WAKE

Ni LAZIMA UFANYE KAZI HARAMU ILI UPATE MAFANIKIO