SALAH AWEKA REKODI MPYA YA MCHANGO WA MABAO KATIKA PREMIER LEAGUE
Mohamed Salah aliweka historia katika Premier League siku ya Jumapili baada ya kufikisha jumla ya mchango wa mabao 45 msimu huu—akiivunja rekodi ya awali ya 44 iliyokuwa inashikiliwa kwa pamoja na Thierry Henry (2002–03) na Erling Haaland (2022–23).
Katika ushindi wa Liverpool wa 2-1 dhidi ya West Ham huko Anfield, Salah alitoa pasi murua ya trivela iliyomuwezesha Luis Díaz kufunga bao katika kipindi cha kwanza. Hii ilikuwa asisti yake ya 18 msimu huu, na anashikilia nafasi ya kwanza kwa idadi ya asisti katika ligi. Tayari pia ana mabao 27 katika msimu huu wa Premier League.
Kwa kasi aliyonayo, Salah sasa yuko njiani kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya msimu mmoja wa mechi 38 wa Premier League kufikisha au kuvuka jumla ya michango 50 ya mabao—hii ni rekodi ya kipekee kwa nyota huyu wa Misri.
Comments
Post a Comment