WACHEZAJI WA REAL MADRID WATOA ONYO KALI
Mchezo wa marudiano unatarajiwa kupigwa Jumatano hii kwenye dimba la Santiago Bernabéu, na tayari nyota wa Real Madrid wametuma ujumbe mzito kwa Arsenal kupitia mitandao ya kijamii.
Jude Bellingham, mmoja wa wachezaji wa kutegemewa msimu huu, alichapisha kwenye ukurasa wake:
“Tutaonana Jumatano, Madridistas!” – ujumbe mfupi lakini uliojaa maana kwa mashabiki wa Los Blancos.
Vinicius Junior naye hakuachwa nyuma. Akiwa na beji ya nahodha, aliandika:
“Tayari nafikiria kuhusu Jumatano!!! Tuko tayari na tunaisubiri kwa hamu. Tutawangoja Bernabéu na tutapambana hadi mwisho. SISI NDIO REAL!!! HALA MADRID!”
Rodrygo alimalizia kwa kusema:
“Tutaonana Jumatano, Madridistas! Nyinyi ni muhimu sana! TWENDE MADRID!”
Kwa upande wa Arsenal, walitawala mchezo wa kwanza kwa mabao kutoka kwa Declan Rice na Mikel Merino, wakijiweka kwenye nafasi nzuri kuelekea nusu fainali.
Lakini kwa historia ya Real Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa – timu yenye rekodi ya mataji mengi – huwezi kuwahesabu nje mapema. Wengi wanasubiri kwa hamu kuona kama kikosi cha Carlo Ancelotti kitaweza kuandika hadithi ya kurudisha matokeo Bernabéu.
Mshindi wa mechi hii atakutana na mshindi kati ya Paris Saint-Germain na Aston Villa kwenye hatua ya nusu fainali.
Je, Arsenal watadumisha uongozi wao au Real Madrid watafufuka kama ilivyo desturi yao? Tuambie maoni yako kwenye sehemu ya comment!
Comments
Post a Comment