KESI YA NICOLE BERRY YAAHIRISHWA: UPELELEZI BADO HAUJAKAMILIKA
Wakili wa Serikali, Rhoda Maingu, aliiambia Mahakama kuwa bado wanakamilisha taratibu za uchunguzi, hivyo wakaomba kesi iahirishwe. Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemalira alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha shauri hilo hadi tarehe tajwa kwa ajili ya kutajwa.
Kwa mara ya kwanza, Nicole Berry na mwenzake walifikishwa mahakamani Machi 10, 2025, wakisomewa mashitaka matatu, mojawapo likiwa ni la kuongoza genge la uhalifu, kosa kubwa chini ya sheria za uhujumu uchumi. Mashitaka hayo yanadaiwa kutekelezwa kati ya Julai 2024 na Machi 2025 katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Mnamo Machi 17, 2025, Nicole alifanikiwa kupata dhamana kwa hati ya nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 100 iliyowasilishwa na mdhamini ambaye hadi sasa jina lake halijafahamika.
Dengah Media TZ itaendelea kufuatilia kesi hii kwa karibu na kukupa taarifa mpya pindi zitakapotolewa.
Kwa habari zaidi za burudani, siasa, michezo na mahusiano – endelea kutembelea Dengah Media TZ.
Comments
Post a Comment