ENG. HERSI SAID APATA TUZO YA KIMATAIFA KUTOKA WORLD FOOTBALL SUMMIT (WFS)

 


Rais wa Klabu yetu na Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu Afrika (Africa Clubs Association - ACA), Mhandisi Hersi Said, ametunukiwa tuzo maalum kutoka World Football Summit (WFS) kama kutambua mchango wake mkubwa katika kuunganisha na kuendeleza ushirikiano baina ya vilabu vya soka barani Afrika.

Tuzo hiyo imetolewa wakati wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa soka – WFS, uliofanyika katika Jiji la Rabat, nchini Morocco

Kupitia nafasi yake kama Mwenyekiti wa ACA, Eng. Hersi amekuwa mstari wa mbele kusukuma ajenda ya maendeleo ya vilabu vya Afrika, ushirikiano wa kiufundi, biashara ya soka, na uwezeshaji wa vipaji kupitia jukwaa la umoja huo.

Tunampongeza kwa heshima hii kubwa ya kimataifa — ni ushindi si kwake binafsi tu, bali kwa klabu yetu, nchi na bara la Afrika kwa ujumla

Comments

Popular posts from this blog

MAJUKUMU YANAWEZA KUMFANYA MUME AKAKOSA MAPENZI NA MKE WAKE

Ni LAZIMA UFANYE KAZI HARAMU ILI UPATE MAFANIKIO