Posts

TANZANIA KUNA WANAWAKE WAZURI SIJUI KWANINI JUX KAENDA KUOA NIGERIA

Image
    Katika kile kinachoonekana kuwa hisia za mshangao na mapenzi ya dhati kwa uzuri wa wanawake wa Tanzania, msanii maarufu Harmonize ametoa kauli kali kwenye ukurasa wake wa Instagram. Akiwa amevutiwa na video za harusi ya Juma, Harmonize ameandika: “MAN I JUST SAW THE VIDEOS OF THE WEDDING, TANZANIAN WOMEN ARE BEAUTIFUL, BOMBCLAAAAAAAT! One can ask themselves, why did Juma go all the way to Nigeria while the light is shining right here at home!” Kauli hiyo imezua mjadala mtandaoni, huku wengi wakikubaliana naye na wengine wakimtetea Juma kwa chaguo lake la mapenzi. Kama ilivyo kawaida ya Harmonize, alimalizia ujumbe wake kwa maneno yenye uzito: “Love is a beautiful thing” Je, una mtazamo gani kuhusu hili? Je, kweli mwanga ulikuwa hapa nyumbani? Toa maoni yako hapa chini na endelea kutembelea Dengah Media TZ kwa habari motomoto kama hizi!

PAPAYA EX AZUA TAHARUKI KWENYE HARUSI YA PRISCILLA OJO – AVAA VAZI LENYE PICHA YA BWANA HARUSI KIFUANI

Image
  Katika harusi ya kifahari iliyofanyika Lagos, Nigeria tarehe 17 Machi 2025, Priscilla Ojo – mwana wa muigizaji mashuhuri Iyabo Ojo – alifunga ndoa ya kitamaduni na mpenzi wake kutoka Tanzania, Juma Jux. Tukio hilo lilihudhuriwa na mastaa wengi wa Afrika, lakini lililowashangaza wengi zaidi ni tukio la Papaya Ex, mrembo maarufu na mjasiriamali wa mitandaoni. Papaya Ex alitinga harusini akiwa amevaa vazi lenye picha ya Juma Jux (bwana harusi) kifuani, na picha ya Priscilla (bibi harusi) kiunoni. Wakati wa sherehe, alitoka na kuanza kumwagia maharusi pesa huku vazi lake likiwa wazi kabisa kwa kila mtu kuona. Hali hiyo ilimkasirisha Priscilla ambaye alimkabili kwa swali, “Kwa nini umeweka picha ya mume wangu kifuani?” Papaya Ex alimjibu kwa utulivu, “Samahani baby, ni kwa sababu nakupenda.” Baadaye alieleza kuwa alifanya hivyo kwa ajili ya kupata attention mitandaoni. Harusi hiyo ilihudhuriwa na mastaa kama Diamond Platnumz, Mercy Aigbe, Peter Okoye, Ebenezer Obey, Femi Adebayo, na w...

JINSI NILIVYOKUTANA NA MUME WANGU JUMA JUX’ – PRISCILLA OJO

Image
 Priscilla Ojo, binti wa mwigizaji maarufu wa Nigeria Iyabo Ojo, amefunguka kuhusu jinsi alivyokutana na mume wake, msanii maarufu wa Tanzania, Juma Jux. Katika video ya mahojiano inayotrend mitandaoni, alieleza kuwa walikutana kwa mara ya kwanza kwenye safari ya kibiashara nchini Rwanda. Alisema: Tulikutana kwenye safari ya kibiashara nchini Rwanda, aliniona kwanza kwenye daraja la biashara (business class), halafu tukakutana tena hotelini. Alinipa namba yake na kuniambia nimtume ujumbe lakini sikufanya hivyo. Lakini baadaye alijua namna ya kunifikia na tukaanza kuzungumza.” Uhusiano wao uliendelea na hatimaye kupelekea harusi ya kitamaduni iliyofanyika Lagos, Nigeria, tarehe 17 Aprili 2025, baada ya kufunga ndoa ya Kiislamu nchini Tanzania mwezi Februari.JP2025: ‘Jinsi nilivyokutana na mume wangu Juma Jux’ – Priscilla Ojo Harusi hiyo imekuwa gumzo kubwa mitandaoni, na baadhi ya watu wakiiita "harusi ya mwaka," huku ikilinganishwa na harusi ya msanii Davido.

HARUSI ZA KISASA, NDOA ZA AIBU – MWAKINYO AVUNJA UKIMYA!

Image
  Bondia maarufu Hassan Mwakinyo ametikisa mitandao baada ya kutoa ujumbe mzito kwa vijana wanaokimbilia harusi za kifahari bila msingi imara wa ndoa. Katika ujumbe wake aliouachia kwenye  insta stori yake  Mwakinyo alisema: "Kabla ya kufanya harusi za vishindo na hasara chungu nzima, hakikisheni na nyie waoaji ni waume kweli mkiwa ndani. Tumechoka na hizo skendo zenu za kukosa magongo!" Ujumbe huu umeibua mjadala mkubwa mitandaoni, wengi wakikubaliana naye kuwa harusi nzuri haiwezi kufunika ndoa isiyo na misingi imara. Mwakinyo anaonekana kuwakumbusha vijana kuwa kuoa si fashion show  ni maisha halisi yanayohitaji uhalisia na uimara wa tabia. Je, wewe unasemaje kuhusu kauli hii ya Mwakinyo? Unakubaliana naye? Tupia maoni yako hapa chini! 👇

YANGA KUMRUDISHA INONGA BAKA JANGWANI

Image
  "Yanga inauhitaji mkubwa wa kusajili mchezaji wa eneo hilo, Ila kuhusu nani anakujani mapema kuzungumza kwa sasa, Lakini mchakato unaendeleana majina ya wachezaji wanatazamwa kwaajili ya kuongeza nguvu eneo hilo tumekuwa tukilifanyia kazi. Kwamuda sasa yapo mezani na tayari yameanza kufanyiwa mchakato jinala Inonga ni miongoni mwao," alisema mtoa taarifa ambaye hakutaka kutajwa jina lake. Klabu ya Yanga SC imeanza mchakato wa kusajili wachezaji wapya kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi chao, huku taarifa zikieleza kuwa kuna uhitaji mkubwa katika eneo fulani (ambalo halijatajwa rasmi). Akizungumza na Dengah Media TZ, mtoa taarifa wa karibu na klabu hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema: Yanga inauhitaji mkubwa wa kusajili mchezaji wa eneo hilo. Ila kuhusu nani anakuja ni mapema kusema kwa sasa, lakini mchakato unaendelea. Majina ya wachezaji tayari yapo mezani na yanafanyiwa kazi. Jina la Inonga ni miongoni mwao." Iwapo taarifa hizi zitathibitishwa, basi ...

YAW SIKI: “SIKUAMINI KURUDI KWA KRISTO MPAKA NILIPOKARIBIA KUFA”

Image
  Maisha Hubadilika kwa Sekunde Moja… Yaw Siki, msanii maarufu wa Ghana aliyegeukia kazi ya uhubiri, amesimulia jinsi ajali ya mwaka 2013 ilivyomfungua macho kuhusu imani yake ya kidini. Katika mahojiano aliyofanya na 3Music TV, alisema kuwa ingawa alikulia katika familia ya Kikristo, hakuwahi kuamini kabisa kuhusu kurudi kwa Yesu Kristo. Nilikuwa namjua Mungu kupitia Kristo, lakini haikuwa imani ya undani. Ilikuwa ni hadi nilipopata ajali mbaya ya gari, nikawa kitandani hospitalini, ndipo nilimuomba kaka yangu aniletee Biblia. Ndipo nilipoanza kumtafuta Mungu kwa moyo wangu wote," alisimulia Yaw Siki. Tangu siku hiyo, maisha yake yalibadilika. Leo hii, anatumia muda wake kuhubiri injili na kuwatia moyo watu wengi kujenga uhusiano wa kweli na Mungu kupitia maandiko. Unajifunza nini kutoka kwa Yaw Siki? Maisha yanaweza kubadilika ghafla — lakini daima kuna nafasi ya kuanza upya na kumkaribia Mungu.

MAMA LUKAMBA AMUWSHIA MOTO BABALEVO

Image